MOURINHO: NATAKA MAKUBWA ZAIDI KUTOKA KWA MARTIAL


KOCHA Jose Mourinho amesema kwamba anataka makubwa zaidi kutoka kwa star wake, Anthony Martial, licha ya kung’ara katika mchezo wa juz ambao Manchester United waliibuka na ushindi dhidi ya Real Madrid.

Msimu uliopita straika huyo alishindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Man Utd, baada ya kuwasili msimu wa 2015-16, lakini usiku huo wa kuamkia jana akaonesha kiwango cha hali ya juu kilichowafanya mabingwa hao wa Ligi ya Europa kupata bao la kuongoza kabla ya kipindi cha pili.
"Ni dhahiri tunataka uwiano zaidi katika kipaji chake, nadhani leo (juzi) ilikuwa chanyamoto kwake, ndiyo sababu nimemwacha kwa muda wa dakika 90 uwanjani, alifurahia na kujaribu vitu," alisema Mourinho.
"Ni muhimu kujaribu vitu katika mchezo wa kirafiki kama huu hivyo ilikuwa ni vizuri kwa Anthony na kujiamini kwake. Yeye bado ni kijana mdogo, bado ana muda wa kujifunza, kujiimarisha na vilevile kujijenga,” aliongeza Mreno huyo.

Alisema anachoweza kueleza ni kwamba, star huyo amefanya mazoezi vizuri zaidi tofauti na mwanzo na amejituma na sasa kilichobaki ni kuonesha kipaji chake zaidi katika njia inayotakiwa.
LihatTutupKomentar