SIMBA YASITISHA KUJENGA UWANJA

Uongozi wa club ya simb umesitisha ujenzi wa uwanja wao unaojengwa eneo ia Bunju jijini Dar es salaam, uongozi umesema umesitisha kwa sababu ya kupata  fedha za kutoa nyasi bandia ambazo zinatakiwa kuweka kwenye uwanja huo, umesema unawataka wanachama wa club ya simba wawe wavumilivu kwani uwanja huo utaendelea muda sio mrefu.
  Uongozi huo umesema  hauwezi kuteteleka kwani fedha za uwanja huo zipo zimetengwa hadi ujenzi huo kumalizika  ifikapo mwakani, Pia timu hiyo ya simba sc club  kwa sasa ipo mkoani  Mwanza ikijiandaa na kucheza na timu ya mwadui katika uwanja wa kambarege mkoani Shinyanga siku  ya jumamosi octoba 29,2016, Kocha wa timu ya simba  Omog akiahidi kumaliza  bila kufungwa, anawaomba washahabiki wa simba kuisapoti timu  yao ambayo kwa sasa inaongoza ligi.
  Timu ya simba kwa sasa ipo katika kiwango kizuri kulingana na  michezo yake ambayo  imeshacheza ikionyesha kiwango cha juu baada ya kufanya vibaya misumu miwili mfululizo, imejiandaa msimu huu kunyakua ubingwa wa ligi ya vodacom.
LihatTutupKomentar