CHELSEA YAVIFUNIKA VIRABU HIVI USAJIRI WA MCHEZAJI HUYU

NYOTA wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ameziingiza vitani timu kubwa zinazoshiriki Ligi Kuu England ambazo zinaisaka saini yake kwenye dirisha litakalofunguliwa Januari, 2020.
Imeripotiwa kuwa timu nyingi kubwa zinampigia hesabu nyota huyo ili kuipata huduma yake kwa sasa.
Chelsea iliyo chini ya Frank Lampard imetenga dau la pauni milioni 120 ili kumshawishi nyota huyo atue jambo linaloamsha vita ya kutosha kwa timu nyingine ikiwa ni pamoja na Liverpool, Manchester United .
Endapo Chelsea itapata saini ya nyota huyo kwa dau hilo inatajwa kuweka rekodi mpya kwa dau la ada ya usajili.
LihatTutupKomentar