MKE WANGU NITAMPATAJE?Sehemu 02

Sehemu 02
Story & Mwandishi

Emmanuel Mkome
+255767372829


Ilipoishia endelea nayo,nilipokuwa kitandani sikupata usingizi kwa haraka maana nilikuwa nawaza safari ya kesho yake  itakuwaje maana nilikuwa nimechoka sana.


Asubuhi na mapema nakumbuka ilikuwa ni jumamosi niliamuka nikaenda dirishani kwa mzee MAKOYE nikagoga dirishani kama mara mbili hivi ndo hakasikia akafungua mlango akanambia bora upumuzike siku ya leo kwa kuwa ni siku ya sabato ilikesho asubuhi nitakupa nauli ya kukufikisha kule unako elekea yani shinyanga,nilitafakari Yale maneno ya mzee MAKOYE nikamwambia ngoja nitembee tu huenda nikapata usafiri wa kuomba iliniweze kufika kule Shinyanga yule mzee MAKOYE akamuita mke wake ambae sikumfahamu jina lake maana lugha waliyokuwa wanatumia nikisukuma ingawa na mimi nilikuwa nakijua kidogo siyo sana,akamwambia mke wake anipe shilingi elfu moja,nilishukuru sana tena sana maana elfu moja miaka 1991 kwa sasa kama mtu akupe elfu kumi.


Mzee MAKOYE alinisindikiza hadi barabarani nikaanza safari yakuanza kuitafuta mjini Shinyanga kwa kutembea kwa miguu tena nilitembea kwa kujiamini sana maana tayari mfukoni nilikuwa na hela kama elfu mbili,ilipofika majira ya saa sita mchana nilianza kusikia njaa Kali sana niliulizia sehemu wanayouza chakula nikaambiwa bado kama kilomita moja na nusu ndo nitafika sehemu ya mgahawa,nilivumilia tu maana nilikuwa sina namna,nilitembea hadi pale maeneo ya mgahawani nilifika nikaagiza wali na maharage nilipomaliza kula nikapumzika kama masaa mawili hivi kisha nikaendelea na safari yangu ya kuitafuta Shinyanga mjini ilikuwa kama saa kumi za jioni hivi.


Nikiwa natembea mara kidogo nikaona gari lilokuwa limebeba shehena ya pamba limeharibika na mafundi wakiendelea kutengeneza,nilipofika kwenye hilo gari nilipunguza Mwendo kidogo niliwasalimia kisha nikaondoka kuna jamaa moja hivi mfupi wenyewe walikuwa wanamuita Mr MAPAMBANO alivyo niona natembea nimechoka sana aliniita akaniuliza nikaanza kumuelezea mwanzo mwisho juu ya safari yangu,Mr MAPAMBANO halisikitika sana kisha akanambia nisubiri wamalize kutengeneza gari wanisaidie usafiri wakunifisha Shinyanga mjini sikukutaa maana ilikuwa inaelekea kuwa usiku.

Nilikaa pale kwenye gari huku nikitafakari namna yakwenda kuishi pale Shinyanga maana sikuwa na ndugu wala jamaa tunae fahamiana nae,nilikaa kama lisaa limoja mwishoe mafundi wakamaliza kutengeneza lile gari tukaondoka kuelekea Shinyanga mjini,gari lilitembea kama kilomita kumi hivi tukaanza kuona mataa kwa mbalj yule Mr MAPAMBANO hakaniambia sasa tunakaribia mjini lakini sisi tunakopeleka hii pamba hatufiki kule mjini,nikamwambia yule dereva anishushe maana toka pale kwenda mjini kulikuwa karibu tu,njliwashukuru sana wale jamaa sana sana Mr MAPAMBANO ambae alionyesha ushirikiano wa hali ya juu sana.


Niliachana na hao jamaa nakuanza kutembea taratibu kuitafuta stendi ya mabus iliniweze kupata mahali pa kulala ilikesho niaze kutafuta Kazi maana tayari nilipokuwa nakusudia kufika nishafika,nilipokuwa nikiendelea kuitafuta stendi ya mabasi........

Itaendelea TENA sehemu 03


.
LihatTutupKomentar