MKE WANGU NITAMPATAJE? Sehemu 01

MKE WANGU NITAMPATAJE?

Sehemu 01
Story & Mwandishi

Emmanuel Mkome
+255767372829

Mwaka 1990 nilimaliza Elimu ya sekondari shule moja iliyopo mkoa wa shinyanga wilaya ya meatu kwa sasa mkoa wa Simiyu,nikaanza kusakasaka Kazi kama ilivyo kawadi yetu wanaume kufanya Kazi niliondoka Meatu pale nakuelekea mkoani Mwanza mwaka 1991 nilipofika mwanza namshukuru Mungu niliangaika ndani ya siku takribani kumi hivi kama sikosei nikapata Kazi  kiwandani.

NIlifanya Kazi pale kiwandani ingawa changamoto za Kazi zilikuwa kadha wa kadha kutokana na mambo ya viwandani yalivyo,mwishoni mwa mwaka 1991 pale kiwandani kulipita fagio la kupunguza wafanyakazi kutokana na hali mbaya iliyokuwa inaikabili pale kiwandani kwa bahati mbaya jina langu lilikuwepo kwenye lile fagio la kupunguza wafanyakazi,nilianza tena harakati za kutafuta tena kibarua lakini sikufanikisha mwishoe  nikaona nihame niende sehemu nyingine nikatafute maisha maana pale mwanza mambo yaliendelea kuwa magumu kila siku.

Ilikuwa siku ya jumatano nilifunga safari ya kutoka Mwanza nakuanza kutembea kuelekea Shinyanga mjini,nilianza safari yangu majira ya saa kumi na mbili za asubuhi,nilianza kutembea taratibu maana nilitembea nikiwa naogopa sana maana kulikuwa na giza bado,niliendelea kutembea mwisho nikaona nipumuzike ilinitafute sehemu niombe kulala maana ilikuwa ishafika usiku tayari,mara kidogo nikaona Lori liliokuwa likitokea mwanza likielekea huko shinyanga nilijaribu kusimamisha lakini halikusimama,nikaona  niachane kwanza na kwenda kuomba sehemu ya kulala nikomae na kuomba usafiri wa kunifikisha pale mjini shinyanga,maana tayari nilikuwa siwezi tena kutembea nilikuwa nishachoka sana miguu inauma sana.

Gafla kidogo lilipita gari la bia nikajaribu kusimamisha na lenyewe likawasha taa tu alikusimama,nikaona masaa yanaenda bora nitafute sehemu mapema ilikusudi nipumzike ili kesho niendelee na safari,nilifanya hivyo nikaenda kwenye mji moja ambao ulikuwa pembezoni mwa barabara nilipofika pale kama kawaida yetu waafrika nikajitambulisha baada ya kujitambulisha pale yule mzee wapale ambae yeye alijitambulisha kama mzee MAKOYE akanambia siwezi kulala nyumbani kwake hadi twende kwa mwenyekiti wa kitongoji hicho kujitambulisha zaidi sikushangaa sana maana niliona ni taratibu tu ya kawaida maana mimi ukizingatia na safiri tu siyo kwamba mimi mwaarifu,nilimkubalia yule mzee MAKOYE tulienda kwa mwenyekiti wa kile kitongoji palikuwa na umbali kama mita 400 hivi,ingawa nilikuwa nimechoka sana na safari ya kutembea kutwa nzima nilivumilia lakini mwishoe tukafika pale kwa mwenyekiti wa kile kitongoji.

Nilianza kwa kuwasalimia japo kiswahili kwao ilikuwa shida sana maana wao walikuwa wanaongea kisukuma kiswahili kwao shida,nilijitambulisha kisha mwenyekiti wa kitongoji kile hakamruhusu mzee MAKOYE nikalale kwake ingawa alitoa angalizo kuwa endapo nikishindwa kuendelea na safari kesho yake itabidi nirudi kwake kumwambia kuwa bado nipo kwa mzee MAKOYE.

Tuliondoka pale kwa yule mwenyekiti wa kitongoji nakuanza kuelekea kwa mzee MAKOYE ambako nilipata hifadhi ya kulala hili kesho niweze kwendelea na safari ya kutembea kuelekea mjini shinyanga,tulipofika pale kwa mzee MAKOYE nilikuta wameniandalia maziwa  mtindi na viazi nikula maana nilikuwa na njaa sana nilipomaliza kula nikaonyesha mahala pa kwenda kupumzika yani kulala,nilipo kuwa kitandani sikupata usingizi kwa haraka maana nilikuwa nawaza safari ya kesho yake itakuwaje maana nilikuwa nimechoka sana.


Asubuhi na mapema nakumbuka ilikuwa siku ya jumamosi.........



Itaendelea tena usikose
sehemu 02
LihatTutupKomentar