YANGA KESHO ITAKWEA PIPA BILA HAWA HAPA


Kesho Jumanne,Yanga itakwenda nchini Botswana kujiandaa na mchezo wa marudiano wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers. 

Hata hivyo, Yanga itaondoka nchini bila ya kuwa na baadhi ya nyota wake wapya wa kigeni kutokana na kukosa vibali vya Caf. 

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa wachezaji hao ambao ni Farouk Shikalo, Mustapha Seleman pamoja na David Molinga wataikosa mechi hiyo kwa sababu mpaka sasa bado hawajapata leseni zao kutoka CAF. 

“Wachezaji hao wataikosa kwa sababu mpaka sasa leseni zao kutoka CAF bado hatujazipata. 

“Kama tutasonga mbele katika michuano hiyo hatua inayofuata ndiyo tutawatumia, kilichosababisha mpaka sasa leseni zao zichelewe ni kutokana na hati zao za uhamisho wa kimataifa (ITC) kuchelewa kuzipata, kwa hiyo hatuna jinsi, kama tutafanikiwa kusonga mbele basi katika hatua inayofuata tutakuwa nao,” alisema Ten

LihatTutupKomentar