MAMBO YA KUIVUSHA YANGA KIMATAIFA NI HAYA HAPA.

HUENDA klabu ya Yanga ikafanya vizuri katika mechi ya marudiano dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana siku ya leo katika mechi ya kimataifa huku mechi ya kwanza timu zote zikitoka sare ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam. Yanga huenda ikafuzu hatua inayofuata kwa kufanya haya yafuatayo 1.Kuwaheshimu wapinzani wao kwa maana ya kutokucheza mchezo wa wazi. 2. Kufanya mashambulizi ya kushitukiza mara kwa mara. 3. Kuepuka kufanya makosa ambayo si ya lazima. 4. Kutengeneza umoja ndani ya kikosi kwa maana ya wachezaji wanapaswa kulinda kwa pamoja pia kushambulia kwa pamoja. 

LihatTutupKomentar