KAKOLANYA NA MANULA WATABEBWA NA UKWELI!


Ifike wakati tunapaswa tufahamu sayansi ya mpira. Juzi niliwasikia mashabiki wa Simba wakisema AISHI MANULA anapaswa adake mechi za kimataifa halafu BENO KAKOLANYA adake mechi za ligi. Ni kauli ambayo ilidhihirisha jinsi gani tulio wengi hatuufahamu mpira. Tangu lini golikipa wa mechi za kimataifa akaakaa benchi?. Golikipa wa mechi za kimataifa anapaswa awe fiti muda wote na ili awe fiti anapaswa acheze mara kwa mara hasa mechi za ligi kuu. Halafu kitu kingine makocha wa wenzetu huwa hawapangi wachezaji kutokana na ukubwa wa jina au umaarufu wake hapana,bali huwa wanaangalia fitness yaMchezaji ambaye hayupo fiti huwa hapangwi kabisa mpaka pale atakapokuwa fiti. Hii ina maana kuwa AISHI MANULA kama ana majeruhi kwa sasa na BENO KAKOLANYA akaendelea kufanya vizuri basi usitegemee atarudi mapema kwenye kikosi cha kwanza itabidi nafasi yake aipambanie haswa mazoezini. Tatizo jingine la wachezaji wetu hasa wazawa si washindani wa namba uwanjani. Wengi wao huwa hawapambani kuhakikisha anakuwa mchezaji wa kudumu kikosi cha kwanza pindi mchezaji wa nafasi yake kuwa amepata majeraha. Tusiende mbali mfano mzuri wa MOHAMED HUSSEIN ambaye kuna kipindi namba yake ilienda kwa ASANTE KWASI    

LihatTutupKomentar