ZAWADI ZA UBINGWA MSIMBAZI BADO HALI SI SHWARI TFF WAFUNGUKA HAYA


MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba zawadi zao bado zinashughulikiwa kwani mpaka sasa bado hawajapewa. 

Simba ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa mwaka 2018-19 na msimu mpya unaotarajiwa kuanza Agosti 23 watakuwa ni watetezi. 

Wlfred Kidao Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa suala la zawadi kwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara bado linafanywa kazi. 

"Bado tunafanyia kazi kuhakikisha tunatatua changamoto hii iliyojitokeza baada ya kukosa mdhamini mwaka jana," amesema Kidao

LihatTutupKomentar