HAWA HAPA WACHEZAJI WATAKAO JIUNGA NA SIMBA LEO


NYOTA saba wa timu ya Simba wanatarajiwa kujiunga leo na timu ya Taifa kwa ajili ya kujaanda na michuano ya Chan wakitokea Afrika Kusini.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaimu Mkuu wa timu ya Taifa, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa wachezaji wa Simba wanatarajiwa kujiunga leo na timu ya Taifa.

"Wachezaji ambao hawajajiunga na timu ya Taifa watajiunga leo na timu," amesema.

Wachezaji ambao hawajajiunga na timu hiyo ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, John Bocco, Hassan Dilunga, Aish Manula, Jonas Mkude na Erasto Nyoni

LihatTutupKomentar