DAVID Molinga amejiunga na Yanga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea AC Lega ya Congo.
Nyota huyu ambaye ni mshambuliaji ni pendekezo la Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye alisema kuwa anakuja kurithi nafasi ya Heritier Makambo aliyetimkia Horoya AC.
Huu unakuwa ni usajili wa usiku kwa Yanga kwani mchezaji huyu alishuka usiku wa kuamkia leo na usajili pia unafungwa leo Julai 31.