MATOLA MGUU NDANI MGUU NJE LIPULI FC



Uongozi wa Lipuli FC umesema kuwa bado haujakaa mezani kuzungumza na kocha, Seleman Matola juu ya kuongeza mkataba mpya kwa ajili ya msimu ujao. 

Akizungumza na MKOMESPIRTNEWS, Ofisa Habari wa Lipuli, Clement Sanga amesema kuwa baada ya ligi kuisha na kumaliza mchezo wa fainai kombe la Shirikisho walimpa mapumziko kocha pamoja na wachezaji. 

"Kwa sasa bado hatujazungumza na kocha wetu Matola kwa kuwa baada ya kumaliza ligi pamoja na mchezo wetu wa FA tulimpa mapumziko hivyo muda ukikamilika tutamuita mezani kuyajenga. 

"Amekuwa mwalimu bora ambaye msimu huu ametufanyia makubwa tunamheshimu na tunamuamini, kikubwa ninachojua bado ni mali yetu kwa kuwa hakuna taarifa mpya ambazo tumezipata juu yake licha ya kwamba tunajua lazima atakuwa anapigiwa mahesabu na timu nyingine," amesema Sanga.

LihatTutupKomentar