Wakati Ibrahim Ajibu akiwa amebakiza miezi michache Yanga tayari kumaliza mkataba wake, inaelezwa vigogo wa Simba wanaendelea kumalizana naye kimyakimya.
Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema wamejidhatiti kuhakikisha anarejea ndani ya uzi mwekundu na mweupe kuhakikisha anacheza msimu ujao akiwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.
Imeelezwa kuwa vigogo hao wako kwenye mipango ya kumrejesha Ajibu huku ikisemekana anaweza akapewa mkataba wa miaka miwili.
Kuna uwezekano mkubwa Ajibu akarudi Simba kutokana na hali ya mpito ambayo Yanga wanapitia hivi sasa.
Tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa hana shida na mchezaji yoyote Yanga anayetaka kuondoka aondoke kwani msimu ujao wamejipanga kufanya usajili wa maana.