SIMBA YAENDELEA KUGAWA DOZI MAPINDUZI CUP


KIPINDI cha pili Simba wanapata bao la kuongoza katika mchezo wa kombe la Mapinduzi linaloendelea visiwani Zanzibar Uwanja wa Amaan.

Rashid Juma dakika ya 84 anamalizia pasi aliyotema mlinda mlango wa KMKM baada ya Claytous Chama kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango.

Rashid Juma ambaye aliingia dakika ya 74 akichukua nafasi ya Shiza Kichuya ambaye alipiga kona tano za Simba walizozipata kwenye mchezo wa leo.

KMKM wanazidi kupambana na kufunguka ili kutafuta bao la kusawazisha kwenye mchezo unaoendelea Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar

LihatTutupKomentar