YANGA YAFUNGUKA KUHUSU USAJIRI WA OBREY CHIRWA AZAM





Baada ya aliyekuwa mchezaji wao, Obrey Chirwa kusajiliwa na Azam FC, uongozi wa klabu ya Yanga umeibuka na kueleza kuwa wao wanafanya usajili kwa mapendekezo ya Kocha, imeelezwa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika, ameeleza kuwa Yanga inafanya usajili kwa mahitaji ya Mwalimu hivyo si sahihi kusajili tu ilimradi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Chirwa kusajiliwa Azam wakati ikielezwa Yanga ndiyo walifanya mpango wa kumtumia tiketi ya ndege Mzambia huyo lakini wakapigwa kete na Azam.

Ilielezwa kuwa Yanga walimrejesha Chirwa ili waje wamalizane naye lakini mambo yamekuwa tofauti kama ambayo ilikuwa imepangwa mwanzo.

Tayari Chirwa ametambulishwa leo na uongozi wa Azam FC na ataanza rasmi kuitumikia kuanzia Nover=mba 15 ambapo dirisha dogo litakuwa limeshafunguliwa.

LihatTutupKomentar