MTIBWA SUGAR WAANZA KIBABE KIMATAIFA


Kikosi cha Mtibwa Sugar kimefanikiwa kuanza vizuri michuano ya Kombe la Shirikisho leo baada ya kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo ya Shelisheli mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa kwanza kwa Mtibwa umeanza na rekodi ya kufunga 'Hat-trick' ya Jaffary Kibaya ambaye amefanikiwa kutumia nafasi ambazo walizitengeneza Mtibwa leo.

Kibaya alifunga bao la kwanza dakika ya 13, la pili dakika ya 36 na dakika ya 60 Kibaya alifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa eneo la hatari na walinzi wa Dynamo.

Katika dakika za lala salama mchezaji Raphael Khamis alifunga bao la 4 na la mwisho ambalo limewafanya Mtibwa Sugar kuibuka kifua mbele na kufanikiwa kutumia vizuri uwanja wa nyumbani hivyo ili waweze kusonga mbele wanatakiwa wasiruhusu kufungwa zaidi ya mabao 2 katika mchezo wa marudio utakaochezwa Desemba 5.

LihatTutupKomentar