MAVUGO APATA SHAVU SASA KUCHEZEA TIMU HII

Aliyekuwa Mshambuliaji wa Klabu ya Simba Laudit Mavugo hatimaye amepta timu ya Kucheza baada ya kukaa nje kwa muda na kukosa timu ya kucheza toka alipoondoka katika klabu yake ya Simba baada ya kumaliza mkataba wake.

Mavugo amefanikiwa kupata timu huko nchini Zambia baada ya timu ya Napsa Stars kufanikiwa kunasa saini yake huku ikielezwa kuwa atakuwa akipata mkwanja mrefu zaidi ya ule aliokuwa akilipwa Simba.

NAPSA Stars ni moja ya Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Zambia na kwasasa imekuwa ikisajili ili kuhakikisha inakuwa vizuri katika msimu ujao wa Ligi kuu.

LihatTutupKomentar