TETESI ZA USAJIRI YANGA

WAKATI washabiki wengi wakiwa bado hawaridhishwi na uwezo wa kipa namba 2 wa Yanga Klaus Kindoki kutokana na kuwa anafungwa magoli ambayo inaelezwa kuwa ni ya kizembe inaelezwa uongozi umeanza kufanya mambo kimya kimya kuhakikisha wanapata kipa haraka.

Japo bado uongozi haujaweka wazi kuwa wanamtaka kipa gani kwaajili ya Kumrithi Klaus Kindoki ila Kwataunit.co.ke imetonywa kuwa Yanga huenda wakatua Kenya kwa Golikipa wa Bandari Fc ya Mombasa Kenya.

Kipa Huyo Ni Farouk SHIKALO ambaye ndiye aliyekuwa kipa bora ligi kuu ya Kenya msimu ulioisha huku pia akiwa kipa namba 2 wa timu ya Taifa ya Kenya.

LihatTutupKomentar