Mazishi ya mmiliki wa klabu ya Leicester City aliyefariki kutokana na ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo nchini Uingereza yameanza kwao nchini Thailand.
Wanajeshi wa kifalme na jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha walishiriki katika maandamano makubwa ya kusherehekea maisha yake yaliyofanyika kabla ya mazishi yake huko Bangkok,
Wachezaji wa Leicester City wanatarajiwa kusafiri nchini Thailand kwa mazishi baada ya mechi yao dhidi ya Cardiff.
Bilionea Vichai alifariki pamoja na wafanyikazi wake wawili, rubani wa ndege aliyokua akisafiria na abiria mmoja baada ya ndege hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa.
Walioshuhudia wanasema ndege hiyo ilikuwa tu imemaliza kuondoka uwanjani pale ilipoanza kuyumba na kuanguka na kuwaka moto.
Jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha washiriki katika msafara wa wanajeshi kabla ya mazishi
Mazishi yake yataanza na kafara ya kuoga ya waumini wa kibudha ambayo yatafuatiwa na sherehe ya siku saba ya kidini.
Mwandishi wa BBC Jonathan Head, mashariki mwa Asia ambaye anafuatilia sherehe hizo anasema kuwa zinafanywa faraghani,
Ndugu na jamaa zake wanatarajiwa kuwasili wwakati wowote kuazia sasa.
Suala la hadhi ya mazishi ni muhimu sana nchini Thailand.
"Wakati wa mazishi haya utaona jinsi vito maalumu vitavyotolewa na mfalme Vajiralongkorn -
Pia amesema ''Watu watafuatilia kwa makini sana hii inaashiria jinsi Vichai alivyokua mashuhuri was.
"Alikua mwanabiasha maarufu, lakini zingine zilikumbwa na utata."
Mwili wa bwana Vichai uliwasili Thailand siku ya Ijumaa kabla ya mazishi yake .
Nusara Suknamai, Kaveporn Punpare, rubani Eric Swaffer na mpenzi wake, Izabela Roza Lechowicz, pia walifariki katika ajali hiyo ya ndege ya Jumamosi iliyopita.
Mabaki ya ndege hiyo iliondolewa nje ya uwanja siku ya Ijumaaa.
Uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea.
Naibu wa waziri mkuu wa Thailand Prawit Wongsuwan,meneja wa timu ya soka ya wanawake ya Thailand na rais wa shirikisho la kandanda la Thailand ni miongoni mwa wageni wanaohudhuria mazishi hayo.
Kwa picha mazishi ya mmiliki wa klabu ya Leicester City aliyefariki kutokana na ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo nchini Uingereza yameanza kwao nchini Thailand.