FC BARCELONA YA SHINDA YASUBILI MPAKA DK ZA JIONI
Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga dakika ya 90 akimalizia pasi ya Sergi Roberto kuipatia Barcelona bao la ushindi ikiwalaza wenyeji, Rayo Vallecano 3-2 katika mchezo wa La Liga jana Uwanja wa Rayo Vallecano mjini Vallecas Teresa Rivero, Madrid. Hilo lilikuwa bao la pili Suarez kufunga jana, baada ya lingine dakika ya 11akimalizia pasi ya Jordi Alba, huku bao la lingine la Barca likifungwa na Ousmane Dembele dakika ya 87 na mabao ya Rayo Vallecano yalifungwa na Jose Angel Pozo dakika ya 35 na Alvaro Garcia dakika ya 57
Vinicius Junior akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 83 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Valladolid kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Bernabeu, kabla ya Nahodha Sergio Ramos kufunga la pili kwa penalti dakika ya 88
Cristiano Ronaldo wa Juventus akionyesha jezi aliyozawadiwa kabla ya mchezo wa Serie A na Cagliari jana Uwanja wa Allianz mjini Torino jana kwa kufikisha mechi 400 za klabu kwenye tano kubwa Ulaya. Juventus ilishinda 3-1, mabao yake yakifungwa na Paulo Dybala dakika ya kwanza, Filip Bradaric aliyejifunga dakika ya 38 na Juan Cuadrado dakika ya 87, wakati la Cagliari lilifungwa na Joao Pedro dakika ya 36
Alexandre Lacazette akinyoosha vidole juu baada ya kuifungia bao la kusawazisha Arsenal dakika ya 82 katika sare ya 1-1 na Liverpool usiku wa jana Uwanja wa Emirates kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England kufuatia James Milner kutangulia kufunga dakika ya 61
Demarai Gray akionyesha fulana yake iliyoandikwa 'Asante Vichai' baada ya kuifungia bao pekee Leicester City dakika ya 55 katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Cardiff City Uwanja wa Cardiff, Caerdydd usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Hiyo ilikuwa ni ishara ya kumuenzi aliyekuwa mmiliki wa klabu yao, Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha aliyefariki dunia wiki iliyopita baada ya Helikopta yake kuteketea kwa moto akitoka kuangalia mechi dhidi ya West Ham United Oktoba 27 Uwanja wa King Power