AZAM FC WATOA TAMKO SIMBA NA YANGA

Uongozi wa timu ya Azam FC, umesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo na kufanikiwa kuchukua pointi tatu ugenini watakapocheza na Kagera Sugar uwanja wa Namfua kesho.

Meneja wa Azam FC, Philip Alando alisema kuwa kila kitu kipo sawa wamefikia hatua nzuri ya kufanya maandalizi hivyo watahakikisha wanaendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo.

"Tupo tayari kwa ajili ya kuendelea kupata pointi tatu muhimu kwa kuwa tunajitahidi kufanya kile ambacho kinatakiwa, kama rekodi itaendelea kusimama ni jambo jema ila tupo tayari .

"Mwalimu anazidi kutoa mbinu kwa wachezaji na kuwafanya waweze kujua kwamba wana kazi kubwa ya kufanya licha ya kutopoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa wachezaji wapo salama, tunawaheshimu wapinzani wetu tutafanya juhudi mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.

Azam wamefanikiwa kucheza michezo 11 kwenye ligi kuu huku wakishinda michezo 8 na kutoa sare michezo 3 bila kupoteza ni vinara wenye pointi 27 kwenye msimamo .


LihatTutupKomentar