PETER MANYIKA ATUA KENYA


Aliyekuwa mlinda mlango wa timu ya Singida United Peter Manyika amejiunga na timu ya Benki ya Biashara ya Kenya (KCB) inayoshiriki ligi kuu, kwa kandarasi ya mwaka mmoja.

Meneja wake ambaye ni baba yake Manyika Peter ambaye ndiye Meneja wake amesema kuwa baada ya Singida United kushindwa kutimiza makubaliano yao mkataba ulivunjika hivyo mteja wake alikuwa huru kujiunga na timu yoyote.

"Mkataba wake ulivunjika hivyo alikuwa huru kujiunga na timu na tunashukuru timu ya KCB ina matawi yake hapa imemfuata na tumesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu," alisema.

 KCB walivutiwa naye baada ya mwaka huu kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika Nakuru nchini Kenya akiwa na Singida United ambapo alisaidia timu yake kushika nafasi ya tatu, ametumika pia timu yaSerengeti Boys, Timu ya Taifa na Simba mwaka 2014/2017.


LihatTutupKomentar