MBONA HAJIONGEZI?
SEHEMU YA 04
na GASPER WA MASTORY
♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡♡
ILIPOISHIA
Ngo ngo ngo ngo!! Mlango ulisikika ukigongwa, Brandon liinuka na kisha kwenda kuufungua....SONGA NAYO.... ‘’oooh angel karibu sana,naona umekuja na mzigo je naweza kukupoea?’’ Aliongea Brandon huku akiutazama mfuko mdogo aliokuwa ameushika angel ‘’sawa tu haina shida’’ ‘’karibu jisikie upo hosteli ya kike’’ ‘’ha ha ha ha ha we Brandon wakikusiia wenzio watachukia unaiitaje hosteli yenu ya kike’ ‘’natania tu bhana,unatumia kinywaji gani?’’ ‘’aah we nawe kila siku unanipaga kinywaji leo nmeshiba nashukuru sana’’ ‘’sawa sawa karibu sana ila hata ukisema nkutengee chai ni sawa tu’’ Brandon aliketi wakiwa wanaendelea na stori mbili tatu angel aliufungua ule mkoba na ndani yake aliitoa saa nzuri ya mshale yenye rangi ya silver ilikuwa nzuri na yenye kung’aa hasa kioo chake’akaushika mkono wa kushoto wa Brandon na kuanza kumvalisha taratibu huku kimya kikiwa kimetanda,Brandon hakuamini aliona kama utani akawa anatabasamu tu.baada ya hapo angel alitoa boksi flani hivi akalifungua taratibu na kisha akatoa viatu katika uleule mkoba viatu aina ya travoter vya ngozi akamshika mguu wa Brandon tena na akawa anamvalisha mguu wa kushoto.sijui alijuaje namba ya mguu ya Brandon kwani kiatu kile kilimtosha vyema kabisa wala hakikumbana Brandon. Baada ya kumvalisha viatu vyote viwili ukimya ulitanda angel alimtazama machoni Brandon akiwa karibu naye kabisa ,angel alitamani kuongea akajikuta ameshindwa kujizuia akajikuta amemkumbatia Brandon tu ghafla bin vuu! huku akimng’ang’ania bila kumwachia Brandon alikuwa ametulia tu akaipitisha mikono yake nyuma ya angel kama ishara ya kukubali kukumbatiwa naye. ‘’ahsante kwa zawadi yako nzuri nmefurahi sana dada’’ Angel alijivuta kidogo akawa wameshikamna mikono huu wakitazamana,hakupenda kuitwa dada na mtu ampendaye. ‘’usijali ahsante pia kwa kuipokea zawadi hii ila kwanini unaniita dada?’’ ‘’samahani kumbe haupendi kuitwa hivyo’’ ‘’hivi Brandon ukinitazama machoni mwangu unaona nini?’’ Brandon kusikia hivyo akaanza kutazama vizuri akiwa anadhani labda kunamdudu kamuingia angel machoni,angel aliumia kuona Brandon hajamwelewa anamaanisha nini akainamisha kichwa chini kwa huzuni. ‘’kwani kitu gani kinausumbua mbona sijakuelewa sory?’’brandon aliuliza ,swali ambalo liligota akilini mwa angel akaona hii indo nafasi yake kusema yanayomsibu ila woga wa ghafla ukamkumba akiwaza ataonekanaje mbele ya kijana huyo.alimtazama tena machoni wakati huu machozi yakiwa yamejaa machoni mwa binti huyu,Brandon akawa anastaajabu tu hakuelewa kabisa angel leo amepatwa na nini ,tena angel akamkumbatia huku machoz yakimtiririka mashavuni. ‘’brandon nateseka juu yako sio siri tena utanisamehe kwa haya nitakayosema nakupenda mwenzio,naumia kila nikuonapo nilitamani niipate nafasi hii nikwambie tu ukweli,wangu nimeona ni mwanaume ambaye unajali maisha yangu na mwema nimeshindwa kujizuia kukupenda wewe kwakweli sipo tayari uwe mbali na mimi nakuhitaji uwe na mimi please nielewe utakavyoweza ila ukweli wangu ndo huo sina kingine la kuficha nmekuweka wazi ili ukiona vyema uniokoe katika mateso haya’’ aliongea kwa hisia kali binti Yule akijivuta na kutazamana macho kwa macho na brandon.
Brandon alimtazama kwa muda kisha akamshika mashavuni angel akimpukuta machozi yaliyokuwa yameshaulowanisha uso mzuri wa binti Yule.amakweli angel alimaanisha alichokisema hakuwa na chembechembe ya masihala katika kila neno lililomtoka binti Yule. ‘’usijali nmekuelewa ila subiri kwanza muda ndio utaamua kwa sasa sina jibu la mojakwa moja la kukupatia kwakuwa nimapema sana kwangu kulitolea uamuzi suala hili,sawa eeh?’’ alijibu Brandon kwa utulivu na umakini mkubwa. ‘’sawa mimekuelewa but please nionee huruma katika maamuzi yako,ila ningependa nikushirikishe kidogo maisha yangu ya nyuma kama upo tayari?’’ ‘’ningependa unishirikishe lakini naona muda sio rafiki itabidi tujiandae si unajua saa 12 tunakipindi na sasa ni saa 11;44, au wewe unaonaje?’’ ‘’ni sawa haina shida wakati mwingine tutazungumza zaidi’’
Baada ya mazungumzo hayo angel alimsubiria Brandon amalize kujiandaa kisha waliondoka wote wakielekea madarasani njiani angel akiwa anaagana na brandon ili akachukue daftari zake mara kwa mbali alionekana Vanessa anakuja upande ule walipo brandon na angel akitokea kwenye hostel zao za kike....alionekana dhahiri ameghadhabika kumuona angel akiwa na brandon.alizidi piga hatua hadi akawafikia walipokuwa wamesimama wanaagana....ITAENDELEA.......haya sasa asipotolewa. mtu manundu mimi naacha kuandika hii story kabisaaa......Nenda kalike page yangu inaitwa simulizi tamu za gasper. huko utazikuta story nyingine nyingi kama. kibuti,mke wa boss,Ugenini.n.k
whatsapp.0656322828.