KOCHA MWINYI ZAHERA AFUNGUKA HAYA KUHUSU BEKI WAKE

Kocha Mkuu wa Yanga ,Mwinyi Zahera amesema kuwa licha ya nahodha msaidizi Juma Abdul kurejea na kuweza kucheza dhidi ya Malindi bado anamuona hayupo fiti kuanza kikosi cha kwanza.

Zahera amesema kuwa chipukizi Paul Godfrey amekuwa akionyesha kiwango kizuri hivyo ataendelea kumtumia kwa muda kwenye mechi ligi kuu.

"Juma Abdul amerejea katika timu na amecheza kwenye mechi ya hivi karibuni ,labda mimi namuona bado sana kumtumia kwenye kikosi cha kwanza ,yeye anakosa mechi fitinesi ndiyo maana nimeamua kumuweka pembeni kwa sasa"alisema.

LihatTutupKomentar