Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars Emmanuel Amunike ameshangazwa na uwezo wa nahodha wa Stars Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kuiongoza timu kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) licha ya kukosa penati.
Amunike amesema kuwa kuna ugumu kwa timu hasa katika safu ya ushambuliaji kwa kushindwa kumalizia nafasi nyingi ambazo wanazitengeneza kwa kukosa umakini.
"Wachezaji wengi wanauwezo mkubwa wakiwa uwanjani kinachowashinda ni umakini katika kumalizia nafasi ambazo wanazipata, nina imani watakuwa sawa katika mchezo unaofuata.
"Mchezaji kama Samatta anaonyesha namna ambavyo anapambana, uwezo wake unaonekana hii inamaanisha kwamba Tanzania kuna vipaji vingi ambavyo vikifanyiwa kazi vitaleta matunda kwenye taifa"alisema