HARMONIZE AOKOA JAHAZI NDANDA FC AMEWALIPIA DENI LA

MSANII wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali, maarufu kama Harmonize ameisaidia klabu ya Ndanda FC kiasi cha Sh. Milioni 3.5 ilipe deni na kuondoka mkoani Singida kuzuiliwa. 
Ndanda FC walizuiwa kuondoka hotelini mjini Singida baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Singida United wakifungwa 3-1 Oktoba 6 Uwanja wa Namfua kwa deni la Sh. Milioni 3.5.
Uongozi wa Ndanda FC ulitoa taarifa ya kuomba misaada kwa wadau mbalimbali wa soka wa mkoani Mtwara kuichangia timu hiyo iweze kulipa deni na kuruhusiwa kuondoka, lakini bahati nzuri iliyoje, Harmonize pekee amemaliza tatizo.


Rajab Abdul Kahali 'Harmonize' ameisaidia Ndanda FC cha Sh. Milioni 3.5 iruhusiwe kuondoka Singida

Na uongozi wa Ndanda FC umetoa shukrani za dhati kwa mwanamuziki huyo msaliwa wa Mtwara,anayemilikiwa na lebo ya WCB Wasafi Record, iliyo chini ya msanii nyota wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Harmonize anayefahamika zaidi kwa wimbo wake Bado aliomshirikisha bosi wake, Diamond Platnumz amekuwa akihudhuria mechi za Ndanda na kujitambulisha kama shabiki wa timu hiyo ya nyumbani kwao.
Ndanda FC inashika nafasi ya 15 katika Ligi Kuu ya timu 20, ikiwa imejikusanyia pointi nane katika mechi nane na kwa ujumla msimu huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu nyingi kifedha kutokana na waliokuwa wadhamini wakuu wa ligi, Vodacom kujitoa.

LihatTutupKomentar