DIAMOND KUANZISHA MASHINDANO MWAKANI HAJI MANARA ATIA NENO

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuanzia mwakani wanaanzisha mashindano ya mguu wa mpira yatakayojulikana kwa jina la Tandale Diamond Super Cup.
Manara ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi jezi pea mbili na mipira kwa Diamond ajili ya kuwagawia vijana wa Tandale.
Amesema anaamini maahindano hayo yataibua vipaji vipya vya wacheza mpira, mchezo ambao umetoa ajira nyingi kwa vijana.
Wakati kwa upande wa jezi amesema wamempa Diamond kama zawadi kwa watu wake wa Tandale ambapo ndiye ataamua awape kina nani.
Naye Meneja wa Diamond, Said Fella Mkubwa Fella amemsifia mama yake Diamond kwa malezi bora.
Fella amesema ni kutokana na hilo ndio maana mambo mengi ambayo wamekuwa wakimshauri Diamond amekuwa akiwasikiliza.
"Malezi kama mnavyojua yanaanzia kwa mzazi, hivyo mama Diamond kamlea vema kijana wake na ndio maana hata leo tunaweza kufanya naye kazi vizuri na tunapomshauri huwa anatusikiliza.

LihatTutupKomentar