BENNO KAKOLANYA ALETA NEEMA JANGWANI


UWEZO ulioonyeshwa na kipa wa Yanga, Benno Kakolanya wa kuisaidia timu yake kupata suluhu dhidi ya Simba Jumapili iliyopita, umemwibua mmoja wa matajiri wa klabu hiyo na kuahidi kumwaga noti Jangwani ili kikosi chao kiweze kukaa kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara hadi mwisho.

Kakolanya alikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Simba, akiokoa michomo ya wazi zaidi ya saba kutoka kwa straika hatari wa Wekundu wa Msimbazi hao, Meddie Kagere, Emmanuel Okwi, winga Shiza Kichuya na kiungo, Cletus Chama.

Japo Simba walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini mwisho wa siku timu hizo ziligawana pointi moja moja, huku Kakolanya akiibuka kuwa nyota wa pambano hilo la watani wa jadi.

LihatTutupKomentar