YANGA YAZIDI KUCHANJA MBUGA , YAILAZA SINGIDA 2-0 TAIFA




Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya SIngida United.

Mabao yote mawili yamewekwa kimiani na mshambuliaji Mburudi, Amis Tambwe katika dakika za 30 na 45+.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka Yanga juu ya kilele cha msimamo wa ligi ikifiksha alama 12 nakuwaacha watani zao wa jadi Simba walio na alama 10.

Katika mchezo huo Mfadhili wa klabu ya Singida United, Mwigulu Lameck Nchemba alikuwa jukwaani kushuhudia timu yake ikiangukia pua kwa mara pili mfululizo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya African Lyon.

Baada ya kibarua cha leo Yanga sasa itaanza maandalizi kujiwinda na watani zao wa jadi Simba kuelekea mchezo utakaopigwa Septemba 30 2018.

LihatTutupKomentar