MASHABIKI SIMBA WAMTAKA MASOUD DJUMA



Kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mbao FC walichokipata jana Simba kimewaibua vikali mashabiki wa klabu hiyo na kufikia kutaka Kocha wao Mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems afungashiwe virago.

Mashabiki hao wenye hasira kali wamezidi kukasirishwa na kitendo cha uongozi wa Simba kumbakiza Masoud Djuma jijini Dar es Salaam bila kuambatana na Mkuu wake mikoani.

Katika mchezo dhidi ya Ndanda FC uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Djuma aliachwa Dar es Salaam ambapo alikabidhiwa majukumu ya kuwanoa wachezaji waliosalia pamoja na kile cha pili.

Maamuzi hayo ya mabosi wa Simba yamewapandisha mori mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake Kariakoo ambapo zaidi ikichagizwa na matokeo ya dhidi ya Mbao FC huko Mwanza.

Kupoteza kwa bao hilo moja kumewafanya mashabiki Simba kueleza kuwa Mbelgiji huyo hajui kucheza na mfumo huku wakishangaa kikosi ghali kama kile kuendelea kukosa matokeo ya kuridhisha.


Wameeleza kuwa Simba ina kikosi kipana na ina kila aina ya mchezaji hivyo si vema akaendelea na majukumu na badala yake wametaka Djuma apewe ukocha mkuu.
LihatTutupKomentar