LIPULI FC IMEPATA SHINDI LEO "ALLIANCE FC WAENDELEA KUGAWA POINT

TIMU ya Lipuli ya Iringa imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibwaga Alliance FC kutoka mkoani Mwanza 1-0 katika mchezo wa mchana Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Miraj Athumani ‘Madenge’ dakika ya sita na sasa Lipuli ya kocha Suleiman Abdallah Matola inafikisha pointi sita baada ya kutoa sare tatu mfululizo katika mechi zake za awali.
Hali ni mbaya kwa Alliance FC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, kwani sasa inafikisha mechi tano bila ushindi, matokeo mazuri kwake yakiwa ni sare ya 1-1 ya African Lyon, tena nyumbani Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.

LihatTutupKomentar