MOURINHO AWATAKA WACHEZAJI WAKE WASIONDOKE.


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameibuka na kuwataka wachezaji wake wawili waendelee kukaa klabuni hapo wasiondoke. Wachezaji hao ni mabeki  Marcus Rojo pamoja na Matheo Darmian ambao wamekuwa wakihusishwa na kuondoka klabuni hapo na kutimkia vilabu vingine. Beki raia wa Argentina Marcus Rojo amekuwa akihusishwa na kujiunga na vilabu vya Everton pamoja na Fernerbahce, huku beki Matheo Darmian yeye akihusishwa kujiunga na vilabu mbalimbali vya nchini Italia. Baada ya kuenea kwa taarifa hizo ndipo kocha Jose Mourinho aliboibuka na kuwataka wachezaji hao waendelee kukaa klabuni hapo.

LihatTutupKomentar