BILIONEA WA ARSENAL KUMWAGA NOTI EVERTON.

Na

 MOSES FRANCIS+255715878724

Aliyekuwa mmiliki wa klabu ya Arsenal bilionea Alishev Usmanov ameibuka na kudai kuwa bado anapendelea kuwekeza katika vilabu mbalimbali barani ulaya. Kauli hiyo ameitoa leo baada ya kuwa zimepita siku chache baada ya kufanikiwa kuuza hisa zake katika klabu ya Arsenal ambazo zilikuwa 30% kwenda kwa mmiliki wa sasa wa klabu ya Arsenal Stan Kroenke. Bilionea huyo raia wa Urusi baada ya kuwa ameachana na klabu ya Arsenal kwa sasa anataka kuelekeza nguvu zake zote kuwekeza katika vilabu vya Everton ya nchini Uingereza pamoja na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani.

LihatTutupKomentar