LIVERPOOL MSIMU HUU INATABIRIKA

Na MOSES FRANCIS
+255715878724

Ligi kuu ya uingereza huwa haitabiriki. Ndio huwa haitabiriki. Bingwa pamoja na timu zitakazomaliza nne bora pamoja na timu zitakazoshuka daraja huwa pia huwa hazitabiriki. Ni rahisi sana kutabiri mechi kati ya Real Madrid na Levante. Ni ngumu sana kutabiri mechi kati ya Stoke City na Manchester united. Mechi za klabu bingwa pia ni rahisi sana kuzitabiri. Mechi kati ya Borussia Dortmond na Olympic Lyon inaweza ikawa ni mechi rahisi kutabirika. Mechi ya fainali ya klabu bingwa kati ya Real Madrid na Liverpool pia ilikuwa ni mechi ambayo ni rahisi tu kutabirika. Urahisi wake uliongezeka zaidi baada ya 
Sergio Ramos kufanya yake kwa Mohamed Salah. Liverpool eneo la katikati walipoteana. Timu nzima ilipoteana. Timu muda mwingi iliutumia katika kujilinda kuliko kushambulia. Trent Anord Alexander, Andrew Robertson na wenzao wa kina Virgil walifanya kazi kubwa siku hiyo. Liverpool ya Jorgen Klopp haikuwa na kiungo mwenye mapafu ya mbwa kama Nemanja Matic, Arturo Vidal au Ngolo Kante. Kiungo wao wa muda wote ni Jordan Henderson ambaye hakuwa na kasi ya kuwazuia kina Luca Modric pale katikati. Mechi ikawa imeisha Liverpool akala 3-1. Habari yao ikawa imeishia hapo. Msimu huu Jorgen Klopp kaingia sokoni  na amesajili viungo wawili wa nguvu. Viungo ambao watacheza nyuma ya Jordan Henderson. Liverpool wamewasajili wanaume wawili wakata umeme pale katikati. Henrique Fabinho pamoja na Naby Keita ni baadhi ya wanaume ambao wataibeba Liverpool mabegani kuanzia msimu huu. Ni wanaume ambao watarahisha kutabiri mechi za Liverpool. Huenda msimu huu ikawa ni rahisi kutabiri mechi kati ya Liverpool na Everton au Liverpool na Manchester united. Liverpool itasumbua msimu huu pale England. Ligi kuu ya Uingereza haitabiriki lakini mechi za Liverpool kuna baadhi zitakuwa ni rahisi tu kutabirika. Tusubiri na tuone.

LihatTutupKomentar