KCCA YAICHAPA AZAM FC 4-2

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imepoteza kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya KCCA katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu ujao.

Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa KCCA, benchi la ufundi Azam FC la iliutumia kama sehemu ya kujiweka sawa baada ya mazoezi makali ya takribani siku 10 kambini nchini Uganda.

Azam FC ilianza vema mchezo huo kwa kujipatia mabao mawili ya haraka, ikianza kufunga la kwanza dakika ya tatu lililofungwa na nahodha Agrey Moris, kwa mkwaju wa penalti.

LihatTutupKomentar