YANGA YAWASHUSHIA ZIGO LA LAWAMA TFF

Yanga: TFF iliwachukua wachezaji wetu 6 zaidi ya Masaa 10 kabla ya Mechi Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amelishushia lawama shirikisho la soka nchini TFF kwa kitendo cha kuwachukua wachezaji wao jana na kukaa nao kwa zaidi ya masaa 10 wakati wakifahamu walikuwa na mchezo mgumu dhidi ya Gor Mahia siku inayofuata. Kwa mujibu wa Mwandila, TFF iliwatoa kwenye kambi ya Yanga nyota sita wa timu ya taifa kwa ajili ya kwenda kupiga picha saa 8 mchana ambapo amesema walirejea kambini saa 7 usiku. Mwandila alikuwa akielezea umuhimu wa TFF kutoa ushirikiano kwa timu hasa zinapoliwakilisha taifa huku akisema kuwa tukio hilo linaweza kuwa limewaathiri kwavile wachezaji hawakupata muda wa kupumzika. Yanga imepoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 3-2.
LihatTutupKomentar