YANGA YAWASAJIRI WAWILI LEO HAWA HAPA

Wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa leo majira ya saa 6 kamili usiku, imeelezwa kuwa uongozi wa Yanga umemalizana na wachezaji wake wawili tegemo.
Beki wa kulia Juma Abdul pamoja na wa kati, Andrew Vincent 'Dante' inaelezwa wamefikia makubaliano na Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kwa kila mmoja.
Hatua hiyo imekuja kufuatia mazungumzo ya muda mrefu baina ya wachezaji na uongozi wa klabu hiyo baada ya hapo awali kuanza kuelezwa wangeweza kutimkia mahala pengine.
Awali Juma Abdul aliviteka vichwa vya habari nchini kwa kuelezwa kuwa alikuwa anahitajika na matajiri wa Chamazi, Azam FC lakini tetesi hizi zikaja kugonga mwamba.
Wakati dili hilo likikamilika, kikosi cha Yanga kipo katika maandalizi ya kukabiliana na Gor Mahia FC katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Julai 29 jijini Dar es Salaam.

LihatTutupKomentar