SIMBA WAZIDI KUIBOMOA YANGA

Imeelezwa kuwa uongozi wa Simba upo kwenye mazungumzo ya kimyakimya na beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani, kwa ajili ya kumsajili.

Tetesi za Yondani kuanza kuhitajika Simba zimeanza tangu msimu wa Ligi Kuu Bara 2017/18 umalizike lakini umekuwa ukikwama kutokana na Yanga kuendelea kumsisitiza aendelee kubaki,

Baada ya mkataba wa Yondani 
 na Yanga kumalizika, uongozi wake umekuwa ukimtaka avute subira kwa ajili ya kusubiria mambo yakae vizuri ili baadaye aweze kuongeza mwingine.

Lakini inaonekana kama Yondani amechoka kuvumilia ambapo inaelezwa amekuwa miongoni mwa wachezaji waliogoma kwenda Kenya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika akidai kupewa mkataba mpya.

Taarifa sasa zinaelewa Mabosi wa Simba walio na jeuri ya fedha za tajiri kijana na Bilionea, Mohammed Dewji Mo, wanaweza wakamalizana na Yondani muda wowote kuanzia sasa ili kumrejesha Msimbazi kwa ajili ya uzoefu wake katika mashindano ya kimataifa.
LihatTutupKomentar