CHELSEA YAKUBALI KUMUUZA EDEN HAZARD ILA KITITA CHAKE NI BALAA

LONDON, ENGLAND. Chelsea sasa wanaonekana kukubali kumwaachia Eden Hazard aende zake.
Kilichopo ni hiki, wababe hao wa Stamford Bridge wanaonekana kufungua milango ya kumuuza Hazard, lakini wakiweka kiwango kikubwa cha pesa, Pauni 200 milioni kwa timu inayotaka kumsajili.
Staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa na Real Madrid kipindi cha karibuni na mwenyewe ameripotiwa kuweka mambo hadharani kwamba anafikiria kuachana na Chelsea kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi.
Real Madrid kwa sasa inasaka mchezaji wa kuja kuchukua mikoba ya Cristiano Ronaldo na Hazard hataki kuiacha fursa hiyo kumpita. Wababe hao wa Bernabeu wamemuuza Ronaldo kwenda Juventus kwa ada ya Pauni 99 milioni.
Chelsea imegundua kwamba Madrid watalazimika kusajili mchezaji na wanamtaka Hazard, hivyo wameamuya kuweka dau la kwanza staa huyo anauzwa Pauni 200 milioni, pesa ambayo ikilipwa itavunja rekodi ya dunia kwenye uhamisho ambayo kwa sasa inashikiliwa na Neymar, aliyenaswa na PSG mwaka jana kwa ada ya Pauni 198 milioni.
Hazard amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake huko Chelsea huku akimwambia kwamba watamlipa mshahara wa Pauni 300000 kwa wiki kama atabaki Stamford Bridge.
LihatTutupKomentar