MTANZANIA WA LEICESTER CITY AITWA SERENGETI BOYS

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemualika mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 ya Leicester City ya England, Anthony Starkie kuja kujiunga na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. 
Taarifa ya TFF usiku wa Jumatano imesema kwamba Starkie anatarajiwa kuwasili Alhamisi mjini Dar es Salaam baada ya kuruhusiwa na Leicester City, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya wakubwa England. 
Atajiunga na Serengeti Boys ambayo inajiandaa kushiriki michuano maalum ya vijana Afrika Mashariki na Katik ijulikanayo kama CECAFA Zonal Qualification.  


Wazi uamuzi wa TFF kumuita kijana huyo unafuatia agizo la Mkurugenzi wa Michezo, Dk. Yusuphu Singo kwamba wafuatilie vipaji vya wachezaji wa Kitanzania wanaocheza nje. 
Singo alitoa kauli hiyo kufuatia mshambuliaji Yussuf Yurary Poulsen, anayezaliwa na baba kutoka Tanga  kuichezea Denmark, nchi ya mama yake kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu nchini Urusi. 
Pamoja na kwamba ilikuwa inafahamika Yussuf aliyezaliwa Juni 15, mwaka 1994 ni Mtanzania na anacheza soka Denmark, lakini hakuwa kuitwa timu yoyote ya vijana hadi anafikia katika kiwango kikubwa na sasa anachezea RB Leipzig ya Ujerumani.

LihatTutupKomentar