LIPULI FC YAMSAJIRI BEKI HUYU KUTOKA NDANDA

Klabu ya Ndanda Fc ya mjini Mtwara imeendelea kukimbiwa na nyota wake baada ya leo beki kitasa Job Ibrahim kujiunga na Lipuli Fc ya mjini Iringa.
Beki huyo aliyewahi pia kucheza Yanga Sc, anaungana na beki mwenzake William Lucian "Gallas" ambaye naye amejiunga na timu hiyo inayonolewa na Seleman Matola "Veron".
Tayari Ndanda imeshaondokewa na wachezaji wake tisa waliojiunga na klabu nyingine, Kagera Sugar ya Bukoba yenyewe imenasa karibu wachezaji watano, Lipuli wawili na Yanga Sc mmoja ambaye ni Mrisho Ngasa
LihatTutupKomentar