AZAM FC YAWATULIZA SIMBA NA KUTWAA UBINGWA

Michuano ya club Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati maarufu
CACAFA Kagame Cup hatua ya fainali imechezwa leo kwa vilabu vya
Simba SC kucheza dhidi ya Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Azam FC kutoka Chamazi.
Azam FC wakiwa katika uwanja wa Taifa dhidi ya Simba SC wamefanikiwa kutetea taji lao la Kagame Cup kwa kuifunga Simba SC kwa magoli 2-1, magoli ya Azam FC yakifungwa na Shabaan Iddi Chilunda ambaye amecheza game yake ya mwisho na Azam FC na baadae anaenda Hispania kucheza soka la kulipwa.
Baadae Simba walipata goli la kusawazisha dakika ya 62 kupitia kwa
Meddie Kagere lakini goli hilo lilidumu kwa dakika 7 pekee na baadae,
Aggrey Morris akaifungia Azam FC goli la ushindi dakika ya 69 na kujihakikishia kuwa Mabingwa wa Kagame Cup kwa mara nyingine tena.
LihatTutupKomentar