Kikosi cha Lipuli FC kikiwa ndiyo kimerejea Ligi Kuu Bara msimu uliopita kimeweka rekodi mpya ya mapato kwa maana ya nafasi.
Lipuli FC imeshika nafasi ya tatu kwa mapato katika msimu wa 2017/18 kikiongozwa na Simba na kufuatiwa na Yanga.
Lipuli FC imeingiza Sh milioni 71.9 kwa mechi zote 30 walizocheza kwa msimu mzima.
Mabingwa wa soka Tanzania, Simba ndiyo timu iliyoingiza fedha nyingi zaidi katika viingilio vya mlangoni wakati wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017-18.
Katika mechi 30 ilizocheza, Simba imefanikiwa kuingiza kitita cha Sh milioni 380.8 ikifuatiwa na Yanga yenye milioni 257.2.
MAPATO YA MLANGONI LIGI KUU BARA 2017-18
Simba 380,867,592
Yanga 257,113,365
Lipuli 71,908,665
Singida 68,939,621
Mbeya 54,766,008
Mbao 51,719,270