JEZI YA ALI KIBA NI KAMA YA RIVALDO.

Na MOSES FRANCIS +255715878724 
 Mwaka 1990 ni mwaka ambao kaburu alikuwa bado anatawala katika ardhi ya nchi ya Afrika Kusini. Nchi jirani inayopakana na Afrika Kusini ambayo ni Namibia yenyewe ilikuwa inapata uhuru kutoka kwa hao hao makaburu wa Afrika kusini. Maisha yanaenda kasi sana. Wakati wananchi wa Namibia wakisherehekia uhuru wao wakiongozwa na rais wao Sam Nujoma pia katika nchi ya Brazil raia wa nchi hiyo pia kuna kitu walikuwa wanakisherehekea. Walikuwa wanasherehekea tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama ( ballod'or) ambayo ilichukuliwa na kijana wao Rivaldo Vitor Ferreira. Ni tuzo ambayo huenda hawataisahau hadi leo Ni miongoni mwa tuzo ambayo imewahi kuchukuliwa na wachezaji wenye umri mdogo zaidi. Kwa kipindi hicho Rivaldo alikuwa na miaka 18 tu. Ni bahati iliyoje. Baada ya kuwa amezurura katika vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Barcelona, Inter Milan, na Olympiacos, Rivaldo alijiandikia historia nyingine mpya katika bara la Afrika. Ni miongoni mwa wachezaji wakubwa barani Ulaya ambao waliamua kuja kumalizia soka barani Afrika. Usishangae ndivyo alivyofanya. January 2012 klabu ya Kabuscorp ya nchini Angola ilitangaza kumsajili mchezaji huyu raia wa Brazil. Ni kipindi ambacho Rivaldo alikuwa kama anakuja cheza mechi za bonanza tu pale Angola. Umri ulikuwa ushamtupa. Mwaka 2012 alikuwa na miaka 40. Uwepo wa Rivaldo tu katika klabu ya Kabuscorps ni faida kubwa. Ni faida kubwa kwasababu baada ya kusajiliwa na Kabuscorps ligi ya Angola ikawa inafuatiliwa na wadau wa soka ambao si raia wa Angola. Pia mechi za Kabuscorps zikawa zinajaza uwanja, jezi nazo za Rivaldo ziliuzwa kama njungu. Kuna mtu kazaliwa Angola ni shabiki wa Rivaldo na hajawahi kumuona Rivaldo live tofauti na kwenye Tv. Ni lazima shabiki huyu aende uwanjani kumtazama Rivaldo. Wakati mwingine soka ni biashara kubwa kama zilivyo biashara nyingine ambazo zinafanywa na makampuni pamoja na taasisi nyingine. Biashara hii ambayo Kabuscorps ambayo waliifanya kwa Rivaldo ni biashara ambayo inataka kufanana na biashara ambayo Coastal Union wameifanya kwa msanii wa kizazi kipya Ali Kiba. Huwa nasikia Ali Kiba ana kipaji cha mpira. Ni kweli huenda akawa anakipaji lakini sitaki kuaminishwa sana katika hilo. Siamini sana kama ndio sababu kubwa iliyoifanya klabu ya Coastal Union imsajili. Kuna kitu kipo nyuma ya pazia. Ali Kiba hayuko fiti. Hawezi akacheza mechi za ligi kuu dakika zote 90. Wakati wa mechi ya tamasha la bonanza baina ya mechi ya team Samatta  na team Kiba nilikuwa namfuatilia Ali Kiba kwa ukaribu zaidi. Wenzake wote wanacheza mechi kila wikendi. Ali Kiba wakati anatazamana na golikipa Juma Kaseja kwenda kupiga penati katika mechi hiyo ya bonanza. Ali Kiba alikosa penati ile. Ali Kiba alikuwa ni mlegevu, hakuwa fiti. Muda mwingi anashinda studio kurekodi nyimbo sidhani kama atapata muda wa kusafiri na timu mikoani kwa ajili ya mechi za ligi kuu. Ni ngumu kwa Ali Kiba kumpanga mnacheza na mechi dhidi ya Azam. Kilichofanyika ni biashara tu kati ya Coastal Union na Ali Kiba. Mimi naishi Tanga jezi ya Ali Kiba inauzwa kama jungu. Na mimi pia ninay
LihatTutupKomentar