BODI YA WADHAMINI YANGA YAMPA ABASI TARIMBA TIMU

Baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, Bodi ya wadhamini ya timu hiyo imemrejesha Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito, Abbas Tarimba kuiongoza Yanga kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi. 

Tarimba atashirikiana na Kamati yake kama ilivyoamuliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika jijini Dar es alaam, Juni 10 2018. Tarimba na jopo lake wanakazi ya kukamilisha zoezi la usajili haraka sasa zikiwa zimebaki siku mbili pekee. 

Mashabiki na wanachama wengi wa Yanga wana imani na Tarimba, Rais wa zamani wa klabu hiyo ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa mwanzo Yanga kupendekeza mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji mwishoni mwa miaka ya 90. 

Hivi karibuni Tarimba alifanikisha kuhuishwa mkataba wa Kelvin Yondani na sasa akiwa mbioni kumalizana na Hassani Kessy.
LihatTutupKomentar