ALISSON RAMSES AJIUNGA NA LIVERPOOL

MBRAZIL, Alisson Ramses Becker, maarufu kama Alisson amekuwa kipa ghali zaidi duniani kihistoria baada ya kujiunga Liverpool kutoka Roma kwa ada ya uhamisho ya Pauni 65.
Usajili huo unafanya Liverpool iwe imetumie kiasi cha jumla Pauni Milioni 174.45 baada ya awali ya kuwasajili kiungo wa Guinea, Naby Keita, Mbrazil mwingine, Fabinho na Mswisi, Xherdan Shaqiri.
Alisson amewasili Merseyside Jumatano na kwenda kufanyiwa vipimo vya afya katika eneo la Melwood, wanakofanyia mazoezi Liverpool.
Amesaini mkataba wa miaka sita kabla ya kupanda ndege binafsi kurejea Italia kukamilisha mapumziko wake. 
LihatTutupKomentar