MISRI WAJITETEA KUA MWEZI WA RAMADHANI NDIO UMESABABISHA WASIFANYE VIZURI

Rais wa Shirikisho la soka nchini Misri EFA Hany Abo Rida anasema kuwa funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan iliathiri kampeni za nchini Urusi.
Kikosi kiliamua kufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan ulioisha siku moja tu kabla ya mechi ya kwanza ya Misri.
Misri ilipoteza mechi zote za kundi lake kwa Uruguay, waandalizi Urusi na Saudia.
'Ramadhan ilituathiri kwa kiwango kikubwa , nilizungumza nao kabla ya kombe la dunia lakini walikataa kutofunga'' , Abo Rida alisema.
''Tulikamilisha mwezi mtukufu wa Ramadhan siku moja kabla ya mechi ya Uruguay lakini , funga hiyo iliwaathiri''.
Abo Rida aliongezea: Naweza kukuhakikishia kuwa mataifa mengi ya Uarabuni yaliwalazimu wachezaji wao kutofunga.
Amesema kuwa EFA imeanza kumtafuta kocha mwengine atakayechukua mahala pake Hector Cuper, ambaye aliachia ngazi baada ya timu hiyo kufeli nchini Urusi.
Hatahivyo wamesema kuwa hawajajaribu kutaka kumuajiri kocha wa Morocco na raia wa Ufaransa Herve Renard.
''Najua kwamba Renard yuko katika kandarasi na Morocco ,hivyobasi hatutamzungumzia, lakini iwapo atasitisha kandarasi yake ama kuwa huru nitaanza majadiliano naye kuongoza Pharaoh'', alisema.
Misri bado haijashinda mechi hata moja licha ya kushiriki mara tatu katika kombe la dunia na sasa imeanza harakati ya kufuzu katika michuano ya kombe la Afrika 2019 nchini Cameroon.
Mabingwa hao mara saba wa Afrika, ambao walikuwa namba mbili 2017 walianza kampeni yao ya 2019 kwa kupoteza kwa Tunisia 1-0.
Kibarua cha pili cha Mafarao hao ni dhidi ya Niger mnamo mwezi September.
LihatTutupKomentar