TETESI ZA USAJIRI ULAYA LEO IJUMAA

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce siku ya Jumatatu. (Sabah - via Talksport)
Chelsea inakaribia kuipiku Real Madrid katika kumsajili kipa wa Roma Alisson katika mkataba ambao unaomthamini mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 kuwa na thamani ya £62m. (Marca - via Metro)
Arsenal inatarajiwa kukamilisha uhamisho wa beki wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos, 30, wiki ijayo. (Star)

Na makubaliano ya dau la £26m ya kumnunua kiungo wa kati wa Sampdoria na Uruguay Lucas Torreira, 22, yanakaribia kukamilika.(Telegraph)
Kiungo wa kati wa Chelsea Jeremie Boga, 21, ameanza mazungumzo ya kuhamia katika klabu ya Itali ya Sassuolo. (Mail)
Ajenti wa beki wa Juventus Daniele Rugani amesema kuwa uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuelekea Chelsea unatagemea iwapo Maurizio Sarri atakuwa mkufunzi katika klabu hiyo ya Stamford Bridge. (Sport Italia - via Sun)
Kiungo wa kati wa Real Madrid Marco Asensio 22, anapanga kuhamia Liverpool ambapo huenda uhamisho huo ukamfanya kuwa mchezaji mwenye pochi kubwa katika historia ya klabu hiyo. (Marca - via Express)
Mchezaji anayenyatiwa na klabu ya Manchester United Milan Skriniar amesema kuwa anafurahi kuwa katika klabu ya Inter Milan na anasema kwamba anataka kusalia katika klabu hiyo.
Beki huyo wa kati amesema kuwa Red Devils ina hamu ya kumsajili. (Radio Expres - via Star)
Afrika nje ya Kombe la Dunia
Wolves inapanga kumnunua beki wa Swansea Alfie Mawson, 24. (HITC - via Mail)
Mchezaji anayelengwa na Newcastle Alphonse Areola, 25, huenda anaelekea katika klabu ya Napoli baada ya ajenti wa kipa huyo kukutana na klabu hiyo ya Serie A. (Tuttosport - via Teamtalk)
Newcastle pia wana hamu ya kumuajiri Andros Townsend lakini Crystal Palace wanataka kulipwa dau la £30m kumuachilia winga huyo mwenye umri wa miaka 26 (Times - via Newcastle Chronicle)
Beki wa kushoto wa Celtic Kieran Tierney anapangiwa uhamisho wa kuelekea Everton ambao wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuchukua mahala pake Leighton Baines (Mirror)
Watford imeikasirisha timu ilioshushwa daraja katika ligi ya Premia West Brom baada ya kuwasilisha ombi la £1m kumnunua Ben Foster, 35. Timu hiyo ilioshushwa dara inamthamni kipa huyo wa zamani wa Uingereza kuwa na thamani ya kati ya £10m na £12m. (Mirror)
Kipa wa Watford Heurelho Gomes, 37, amefichua kwamba kuna uwezekano wa yeye kuondoka katika klabu hiyo msimu huu(ESPN Brasil - via Mirror)

Manchester United wako tayari kumsaini kipa wa klabu ya Stoke ,35, Lee Grant. Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Uingereza kisichozidi umri wa miaka 21 atatumika kama kipa wa ziada kwa David de Gea na Sergio Romero. (Telegraph)
Mchezaji wa klabu Everton na nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney, 32, atatia saini mkataba wa miaka miwili na klabu ya DC United katika kipindi cha saa 36 . (Sky Sports)
Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho, 26, anadai kwamba mchezaji huyo anakaribia kukamilisha uhamisho wake hadi Manchester City kwa dau la £43m . (Mirror)
Crystal Palace imempatia kocha Roy Hodgson kandarasi mpya ambayo itamweka katika klabu hiyo hadi 2020. (Sky Sports)
Everton inamnyatia mshambuliaji wa Croatia katika kombe la dunia Ante Rebic. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anaichezea klabu ya Eintracht Frankfurt. (Mirror)

Southampton inakaribia kumsajili mshambuliaji wa basel na Norway Mohamed Elyounoussi, 23. (NBC)
Klabu hiyo pia ina hamu ya kumsajili kipa wa Manchester City Angus Gunn, 22, katika mkataba ambao unaweza kufika dau la £15m. (Mail)
Ujerumani watupwa nje ya Kombe la Dunia
Manchester City haitaangazia kifungu cha ununuzi cha kandarasi ya mchezaji wa Huddersfield raia wa Australia Aaron Mooy , 27 . (Manchester Evening News)
Kungo wa kati wa Argentina na West Ham Manuel Lanzini, 25, anasema kuwa anatarajia kupona kutoka katika jeraha lake la goti kufikia mwanzo wa 2019. (Fox Sports) 
Liverpool imemsajili mshambuliaji wa Uingereza wa timu ya vijana Bobby Duncan, 17, kutoka Manchester City. Duncan ni binamu wa aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Steven Gerrard. (Liverpool Echo)
LihatTutupKomentar