AZAM YAZIDI KUJIIMARISHA YA NASA MWINGINEE

Klabu ya Azam FC imefanikiwa kuinasa saini ya beki Nicolas Wakiro Wadada ambaye alikuwa Nahodha Vipers ya Uganda pia mchezaji wa The Cranes wakati wa michuano ya CHAN.
Wadada ametua Azam ikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea michuano ya KAGAME CUP 2018, inayotarajia kuanza June 28 mwaka huu katika viwanja viwili tofauto vya Azam Complex (Chamanzi) na Uwanja wa Taifa- Dar es salaam.
Usajili huo wa Wadada unakuwa ni usajili wa tano wa Azam Fc katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu wa 2018/2019.
Wengine ambao Azam Fc tayari imewasajili ni Donald Ngoma kutoka Yanga Sc, Tafadzwa Raphael Kutinyu kutoka Singida United, Ditram Nchimbi kutoka Njombe Mji iliyoshuka daraja na Mudathir Yahya kutoka Singida United.
LihatTutupKomentar