ARGENTINA YA PIGWA KIPIGO CHA MBWA KOKO

Croatia imeikunguta Argentina 3-0
Matokeo haya hayakutabiriwa.
Messi aliingia mchuano huu akisaka goli lake la kwanza kombe la dunia 2018.
Hata kuwepo kwa Dybala, Higuain na Messi haikuzalisha bao.
Ni nahodha mmoja tu kati ya Messi na Modric ameng'aa kwenye ngarambe hiyo - ModModric .
Magoli matatu kipindi cha pili yakiwemo mawili ya kuvutia yametosha kupunguza nafasi za Argentina Kombe la dunia 2018.
Kipa Willy Caballero alifanya kosa dakika ya (53) na Ante Rebic hakuchelea kuipa Croatia uongozi.
Croatia ilizidisha uongozi wake kupitia Luka Modric dakika ya (81) na kuzamisha matumaini ya Argentina.
Ivan Rakitic aliweka kando urafiki wake na Messi na kuudunga msumari wa mwisho kwenye jeneza la Argentina kwa kufunga goli la tatu na la mwisho kwenye mechi dakika ya (91).
Hata baada ya kuvua koti lake, hali haikubadilika kwa kocha wa Argentina Jorge Sampaoli.
Kila mmoja sasa anasubiri kauli za Maradona kufuatia udhalilishwaji dhidi ya Croatia.
Mchuano mwingine wa Kundi D, utagongwa siku ya Leo kati ya Nigeria na Iceland.
Croatia itakwatuana na Ufaransa au Denmark hatua ya muondoano.
LihatTutupKomentar